Thursday, August 20, 2009

mtafaruku kidogo...

wakati mwingine ni vigumu kujua watu wanafikiria nini kati vichwa vyao. wewe unasemaje?

ukianza mbio: wewe ni msichana, ukishinda mbio: hatunauhakika na jinsia yako.

pichani ni mshindi wa mbio za mita 800 na ni rekodi kwa mwaka huu kwa wanawake.

kwa ushindi wake huo swala la jinsi a yake limeanza kuingilia kati. je, unadhani kwa ushindi wake swala la jinsia linaingilia kati ili avuliwe ushindi? kwa nini uchunguzi wa jinsia yake haukufanyika kabla ya mashindano? kwa nin IAAF ilimruhusu ashiriki huku ikijua vigezo kama vile sauti yake, maumbile yake ya misuli n.k.. vilikuwa tayari vinaonyesha utata? ukisoma http://en.wikipedia.org/wiki/Caster_Semenya inaonyesha uchunguzi ulifanyika lakini matokeo hayakutoka. sasa ameshinda wanadai uchunguzi tena.

leo jioni atapanda jukwaani kuchukua medali yake ya dhahabu. je, atapata?

hapo kuna utata. we unafikiriaje?

No comments: