Friday, April 03, 2009

mwanamke amtaliki mumewe kwa kuwa msafi zaidi ya mmno.

kuwa msafi mmmmmno kuliko zaidi ya kawaida nomaaaaaaaa....................

Berlin - Ujerumani - mwanamke mmoja wa kijerumani amemtaliki mumewe kwasababu ya kuchoshwa na mumewe kusafisha kila kitu ndani ya nyumba.

taarifa kutoka vyombo vya habari vya ujerumani vimeripoti kuwa mwanamama huyu amekuwa katika ndoa yake kwa miaka 15 akivumilia upenzi wa mumewe wa kufanya kazi ndogo ndogo za usafi za nyumbani kama vile kurudisha vitu mahali pake na kupanga fenicha.

mwanamke huyo alitokwa na uvumilivyu pale alipoona mumewe kavunja na kujenga ukuta ndani ya nyumba yao ambao ulikuwa mchafu. Christian Kropp, hakimu katika mji wa Sonderhausen, alisema alhamisi.

"sijapata kuwa na mtu akitafuta talaka kwaajili ya hili." alisema.

imeripotiwa na fransiska scheven, kuhaririwa na myra macdonald na kutafusiriwa na heri

source: http://www.reuters.com/article/oddlyEnoughNews/idUSTRE5314I620090402

No comments: