Friday, July 04, 2008

mwanaume ajifungua huko marekani

yule mwanaume mmarekani thomas beatie (34) ambaye alikuwa mjauzito mejifungua mtoto wa kike hapo jumapili tarehe 29 - 06 - 2008. wote mama (mwanamme huyu) na mtoto wake wanaendelea vizuri.bibi/bwana thomas beatie alizaliwa mwanammke (alikuwa na jinsia zote mbili ya mwanamke ikionekana zaidi). baadaye aliamua kufanyiwa operesheni na kuwa mwanamme akiwa na miaka 20. operesheni hiyo ilihusisha pia kuondoa matiti lakini kubakiza viungo vya kizazi. aliamua kubaki na viungo vya kizazi kwa kuwa alitamani siku moja kuwa na mto

to wake mwenyewe. tangu mwaka huo alitambuliwa kisheria kuwa yeye ni mwanamme. alioa (~miaka 5 iliyopita) lakini mke wake hakuweza kushika mimba kwa kuwa ni tasa. bwana thomas aliamua kushika mimba kwa njia ya kupewa mbegu za kiume kutoka kwa mtu asiyejulikana hospitali na kuweza kuitunza mimba hiyo mpaka alipojifungua mtoto wa kike tarehe hiyo. taarifa zinasema alijifungua kwa njia ya kawaida lakini kuna tetesi kuwa alijifungua kwa njia ya operesheni.

sasa haijulikani kama ataitwa mr. thomas beatie (kama mume wa mtu), mrs thomas beatie (kama mtu aliyejifungua na ni mama wa mtoto) au vyote (kama mume wa mtu na mama wa mtoto) kutegemeana na wakati. pia mtoto atamwitaje baba, au mama, au babamama au bamabama etc ?

soma http://www.malepregnancy.com/ kwa kumjua mwanaume wa kwanza kujitangaza mjamzito.

kwa habari za kitaalamu zaidi soma: http://en.wikipedia.org/wiki/Thomas_Beatie#Pregnancy_among_intersex_and_transgender_people (kumbuka wikipedia haiko 100% sahihi kwa kuwa kila mtu anaweza kuweka taarifa etc zake)

kutoka live science: http://www.livescience.com/health/080328-pregnant-man.htmlNo comments: