Friday, June 20, 2008

mchungaji wa kianglikana aoa mwanaume mwenzake.

huyu ndiye askofu wa kianglikana huko new hampshire ambaye anawachanganya viongozi wa kanisa hilo (nje na baadhi ndani ya marekani) kuamua kufunga ndoa ya kiserikali (civil union) na mwanaume mwenzake. amekaa na huyo "mchumba" wake kwa miaka 20 na sasa ameamua kuhalalisha. yeye ndiye askofu wa kwanza kujitangaza kuwa ni homosexual. je kanisa litamtenga au kuwatenga wale wanao m"sapoti"?
________________________________________________
cha msingi kutokana na mawazo yangu ni kuwa huyu askofu hakubaliani na msimamo wa imani ya kanisa lake analoliongoza ya kuwa ndoa ni muunganiko wa hiari kati ya jinsia mbili tofauti kwa hivyo kuamua kufuata tamaa zake na kwenda serikalini kuhalalisha ushenzi wake. mimi naona huyu askofu hana dini na hajui kama Mungu yupo ndio maana ameweza kufanya mambo yasiyo mpendeza Mungu. Ninawasihi waumini wote wa dini zote wasiige mfano wa huyu "askofu". pia kwa kuwa waanglikana wa usharika wake au sehemu yake anayoiongoza wamemkubali tusishangae kuona ndoa hizo sasa zinaanzwa kufungwa makanisani. lazima tuombe sana tabia hii chafu ikome. hii si mipango ya Mungu kwa wanadamu.

kutoka kushoto ni mchg. gene robinson, mmoja wa binti yake ella, na "mchumba wake Mark Andrew. kinachonishangaza ni huyo binti kufurahia hatua ya baba yake.


mark andrew ("mchumba") akimkumbatia gene robinson baada ya kuwekwa wakfu 2003.

ndoa ya kiserikali iliyofanyika kwa siri kati ya gene robinson (kulia) na mark andrew (kushoto). picha hii imepatikana kwa msaada wa episcopal dioceses ya new hampshire. msajili wa ndoa hiyo alikuwa ronna wise (katikati) na sherehe hiyo ilikuwa concord, n.h. jumamosi ya tarehe 7 juni 2008. muungano huo ulifanywa kuwa halali tangu tarehe 1 januari 2008

No comments: