Saturday, June 07, 2008

hillary clinton kajitoa kinyang'anyiro cha urais kumwachia baraka zote baraka



hatimaye hillary clinton atamka wazi kumsapoti baraka obama kuwa mgombea uraisi wa chama cha demokrat huko marekani. licha ya kuwa hakutarajia kufanya hivyo. lakini alilazimika kufanya hivyo ili kusaidia kuwang'oa republican kutoka white house. spichi ilikuwa nzuri na kwa mawazo yangu imegusa pembe zote muhimu.


mimi binafsi nilikuwa njia panda. niliwapenda wote yaani hillary na baraka wote wawe maraisi. kwa hivyo yoyote ambaye angechaguliwa na chama ningempenda tuu. wote wawili walikuwa wanaandika historia mpya marekani. hillary alikuwa anaandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kugombea uraisi na baraka ni mgombea wa kwanza mweusi (ukweli ni kwamba baraka ni nusu mweusi na nusu mweupe) lakini mimi nafurahi sana wanavyo mwita mweusi kwa kuwa anatuwakilisha kikamilifu zaidi.


wakati hillary anatoa speech yake hakuwa na furaha niliyozoea kumwona nayo. lakini ninategemea yote aliyosema yametoka moyoni mwake na si kwa kulazimishwa na watu au chama. pia nilisikitika sana kwa kuwa baraka mwenyewe hakuwepo wakati anaachiwa manyanga. ila nategemea kusikia speech ya baraka soon.


cha muhimu kwa sasa ni republican watoke ili vita iraki na kwingineko iishe. pia matatizo ya ndani yaishe pia. kwa mtazamo wangu sioni umuhimu wa kwenda vitani iraq na kutumia mabilioni ya dola kila siku mwezi wakati ndani ya nchi watu hawana huduma nzuri ya matibabu na watu wanalazimika kupita njia mbadala kama jamaa mmoja ambaye alifanyiwa operesheni kwa msaada ya kutoa kansa ya shingo ambayo baadaye ilirudi na akalazimika kuoa (yaani mwanamke alimwonea huruma sana na wakaoana) ili aingie kwenye bima ya afya ya mke wake. pia shida ya madeni ya nyumba, watu wanashindwa kulipia nyumba zao na wanatimuliwa ndani bila kujali watoto n.k.


sasa kazi iliyo baki ni kumsapoti baraka obama yaani democrats wote ili waingie ikulu novemba. muhimu zaidi ni hillary mwenyewe kusaidia kampeni za obama na kubadilisha mtazamo wake kwa baraka na kujaribu kufuta lawama, madongo na mizozo yote waliyokuwa wakitoleana wakati wa kampeni zao. hii itakuwa muhimu kwa kuwa wafuasi wa hillary ni muhimu sana kwa baraka ili ashinde kiti cha uraisi. kwa hivyo lazima wageuzwe kimtazamo ili wamsapoti baraka ambayo ni kazi nyingine kubwa sana.

No comments: