
katika juhudi za kuiokoa dunia yetu wajerumani wameamua kuacha kuuza balbu tulizozizoea na watumiaji watahitajika kununua balbu zinazo tumia nishati kidogo. Pia katika harakati za kuiokoa dunia hii, kuanzia mwaka huu magari yote yamekagulia na kupewa stika maalum ya utambulisho kuwa gari linafaa kuingia kati kati ya mjini. stika ya kijani maana yake ruksa kuingia mjini, stika ya njano kwa mwaka huu ni ruksa lakini baada ya miaka kadhaa marufuku na stika nyekundu ruksa mwaka huu na mwakani hakuna kuingia mjini. yeyete atakaye vunja amri hii atalipa faini kubwa.



hii ni alama ya barabarani ambayo inakutaarifu unaingia zoni ya kutunza mazingira.
No comments:
Post a Comment