Wednesday, August 12, 2009

Ijue Uingereza

Uingereza ni moja wapo ya nchi zinazo tengeneza "Ufalme wa Muungano" (United Kingdom). Nchi zingine ni Uskoti (Scotland), Welisi (Wales) na Eire ya Kaskazini (Northern Ireland). Bendera yao iliunganishwa kama picha inavyoonyesha hapo chini. Unaweza kufika Uingereza kwa njia zifuatazo; kwa ndege kutoka mabara mbali mbali, kwa meli pia kutoka mabara mbali mbali, kwa treni kutokea Ufaransa na kwa njia ya magari (pamoja na mabasi) kutokea Ufaransa pia. Njia ya treni na magari hupitia chini ya bahari kwenye "shimo" liitwalo "Channel Tunnel" lilianza kutumika mwaka 1994 November kwa huduma ya abiria. Shimo hilo lina urefu wa kilometa 50,45 na linaanzia Ufaransa, Calais na kuishia Uingereza, Folkestone - Kent. Shimo hilo limechimbwa katikati ya miamba chini ya bahari ya " English Channel" na kina kirefu kabisa cha bahari hiyo ni mita 180.


Kuvuka bahari hii kwa treni ni kama dakika 20. Huwezi kuona kitu kizuri sana zaidi ya giza nje ya treni. Hapo chini ni Treni iendayo kasi ya kampuni iitwayo Eurostar ambayo hufanya safari zake kila siku kati ya Uingereza na Ufaransa.


Pichani ni Kituo cha mwisho cha Eurostar Uingereza kiitwacho St. Pancras, London.

No comments: