Tuesday, November 25, 2008

sheshe la winter limeanza.........

......... hata kabla ya winter yenyewe haijaanza rasmi. tuombe Mungu isitufunike.
wanafunzi wakitengeneza mpira wa theluji wakati wa mapumziko.


usafiri wa jirani ukiwa thelujini.
usafiri wangu. bahati nilibahatika kukumbuka kufunika na kava ili kiti cha baiskeli yangu kisiwe barafu. siku hiyo nilienda mzigoni nayo. inabidi uwe mtaalamu wa kuendesha baiskeli kwenye barafu.

barabara. asubuhi saa 1.

mdau wa blogu hii akiwa nurnberg ambako palikuwa na theluji nyingi kuliko augsburg.

nilienda nurnberg kuthibitisha theluji kuwa mwaka huu imeanza mapema kuliko miaka miwili iliyopita. pengine mwaka huu ni global cooling :)

hapo unaona maua ngangali na maua ambayo hayamudu baridi kali.

theluji ikiwa imeyayuka baada ya magari kupita.

hii ni cha mtoto. nilishindwa kupata picha nzuri wakati baadhi ya magari yakiwa na kama sm 15 za theluji juu yake.

No comments: