Saturday, September 06, 2008

ijue uingereza

kama inavyofahamika pia kwa jina maarufu UK, ni muunganiko wa england, scotland na wales. pia sehemu ya kaskazini ya ireland pia ni sehemu ya UK. wengi tunaifahamu UK kwa jiji la london ambalo liko england. soma zaidi http://www.woodlands-junior.kent.sch.uk/customs/questions/britain/britain.htmnjaa iliuma sana wakati wa ziara hivyo nililazimika kula pitza ya kimarekani yenye mkate mlaini kwenye hoteli inayo itwa pizza huts pale basingstoke. http://en.wikipedia.org/wiki/Basingstoke


chakula cha asili cha wakaaji wa whitchurch kijiji cha hampshire.

winchester cathedral http://en.wikipedia.org/wiki/Winchester#Cathedral
winchester iko mmkoa wa hampshire. http://en.wikipedia.org/wiki/Winchesterhiyo ni kofia la chuma http://en.wikipedia.org/wiki/Diving_helmet ambalo lilivaliwa na mzamiaji wa kwanza kabisa duniani. kofia hiyo iko maonyeshoni winchester cathedral. ilitengenezwa na augustus siebe http://en.wikipedia.org/wiki/Augustus_Siebe


"bar" ambayo binti yake clinton alikuwa akila sandwich zake. sandwich za hapo ni tamu sana. bar hii iko oxford. http://en.wikipedia.org/wiki/Oxford
ndani ya mazingira ya exerter college. kwa wale wapenzi wa sinema ya harry potter hilo jengo ndipo walipo igizia hospitali.


nje ya jengo la exeter college. ni moja ya vyuo vinavyounda chuo kikuu cha oxford. linki hii ni huo mji http://en.wikipedia.org/wiki/Exeter, na hii ni ya chuo http://en.wikipedia.org/wiki/Exeter_College,_Oxford

baadhi ya vijiji vya hampshire ambavyo baadhi ya nyumba zimeezekwa kwa nyasi.

nilivinjari pia moja ya shule za zamani za mji wa london. hapo nadhani mambo ya afya yamepita mmbali kidogo. kushoto ni sehemu ambapo wanafunzi wanakunywa maji wakati wa mapumziko. kulia ni mambo ya maji machafu kutoka pendine chooni? kwa hivyo hata nchi zilizo endelea mambo kama hayo yapo.hilo ndilo hekalu la malkia wa wingereza akiwa london, Buckingham Palace http://en.wikipedia.org/wiki/Buckingham_Palace
jengo la bunge la wingereza. http://en.wikipedia.org/wiki/Parliament_of_the_United_Kingdom. humo ndio kuna hoouse of lords na house of commons.
nilipata nafasi ya kusafiri na kampuni ya treni southwest trains http://en.wikipedia.org/wiki/South_West_Trains


londo eye ukipenda jicho la london ni gurudumu la tatu kwa ukubwa duniani na ni pekee lenye sapoti upande mmoja. http://en.wikipedia.org/wiki/London_eye

ndani ya london eye

dala dala za waingereza. aina hii ya mabasi hadimu sana sasa. na kama ukilikuta ni kwaajili ya watalii tuu.njaaaaa jamani. hiyo menyu ni nyama iliyokatwa kama kitambaa kisha ikapikwa kidogo (semi-mbichi) na inaseviwa ikiwa ya baridi. nadhani tunaanza kurudi hukoooooo kabla evolution haijaanza. pia inakuja na ndoo ya chipsi.

jengo la kiwanda cha zamani cha kusuka nyuzi na kutengeneza vitambaa aina ya silk. http://en.wikipedia.org/wiki/Whitchurch_silk_mill

treni ya eurostar ambayo inapita kwenye handaki chini ya bahari (english channel)http://en.wikipedia.org/wiki/Channel_tunnel


umesha wahi kusikia msemo huu "mind the gap"? usafirii wa underground jijini london. kutoka kituo kimoja mpaka kingine kwa tiketi ya kawaida ni paundi 4 na senti kadhaa. pengine ukiambiwa daladala dar nauli ni tsh 500 usilalamike kabisa.


hilo ndilo daraja linaloitwa tower bridge. http://en.wikipedia.org/wiki/Tower_bridge

ukiangalia picha hii kwa makini utaona kibanda cha machinga akiuza bidhaa za kitalii. asilimia 95 ya watu unao waona hapo ni watalii.

hilo ndilo kanisa ambalo alkia au mtu yeyote wa familia ya kifalme huwekwa wakfu au hufanya shughuli ya kikanisa. linaitwa westminster http://en.wikipedia.org/wiki/Westminster_abbey ukitaka kutembelea ndani kama mtalii mtu mzima ni paundi 12 na watoto no paundi 9. unaweza ukakutana na malkia akiwa anasali. jaribu bahati yako.

No comments: