Friday, March 07, 2014

dunia imeponea chupuchupu kwa asteroid (kiswahili ?) kupita karibu

kwa sasa nita tafsiri asteroid kuwa jiwe kubwa.

jiwe kubwa (linaitwa 2014 dx110) limepita karibu kabisa na dunia umbali mfupi kidogo kulinganisha na umbali ambapo mwezi upo. jiwe hilo limepita karibu na dunia umbali wa kilometa 350,000 kwa spidi ya zaidi kilometa 53,000 kwa saa. spidi hii ni sawasawa na mara 300 ya spidi ya gari linalo endeshwa kwa spidi ya kilometa 180 kwa saa. kama jiwe hili lingeigonga dunia (kuanguka duniani) lingetengeneza shimo lenye kipenyo cha mita 600. jiwe hilo linaukubwa wa kipenyo mita 30. mwezi uko umbali wa kilometa 384,400 kutoka duniani. matukio ya mawe haya yataendelea kutoke mpaka machi 16. hivyo angalia anga kwa mawe mengine wakati wowote ikiwezekana andika urithi mapema.

soma zaidi kupitia viunganishi hivi

http://rt.com/news/asteroid-flyby-earth-moon-783/

http://www.dailymail.co.uk/sciencetech/article-2572908/Asteroid-race-past-Earth-tomorrow-YOU-watch-live-online.html

http://metro.co.uk/2014/03/05/dont-panic-but-theres-a-massive-asteroid-passing-between-the-earth-and-the-moon-tonight-4426627/

Friday, December 06, 2013

P. K. A. (RIP)

Tafsiri:

Hakuna mtu aliyezaliwa akimchukia mtu mwingine kwa sababu ya rangi ya ngozi yake au dini yake. Watu lazima wajifunze kuchukia, na kama wanaweza kujifunza kuchukia basi wanaweza kufundushwa kupenda, kwa sababu kwa kawaida upendo huja miyoyoni mwa watu kuliko kinyume chake.

Nelson Mandela

Sunday, November 03, 2013

twendeni "global"

 
angalau hata wa ulaya wanaburudika kitanzania na tanzi shakers.
 

(samahani kwa kwaliti mbaya ya video hii)

Wednesday, October 16, 2013

nyoka, moto na biblia

  • ni dini huko marekani.
  • kuna makanisa zaidi ya 100
  • wachungaji wanaani siku ikifika imefika.
angalia hapa (kiingereza)
http://www.youtube.com/watch?v=g5O1RVWB8MQ

Sunday, October 06, 2013

unene na uraia huko new zealand.

(tafsiri kamili baadae)

raia mmoja kutoka afrika ya kusini amenyimwa kibali cha kuishi new zealand kwasababu ni mnene mno (kilo 130 tuu)

soma zaidi (kwa kiingereza)
http://www.bbc.co.uk/news/world-asia-23475583